Thursday, 16 February 2017

Fahamu namna ya kuandaa juisi ya limao ili kumaliza mafua makali

Mafua ni ugonjwa ambao chanzo chake ni kuathirika kwa mirija ya kichwani ya mfumo wa kuvuta pumzi. Athari hizo huletwa na virusi vya aina mbalimbali kupitia kwenye hewa au vumbi na ni ugonjwa unaoambukizwa kwa haraka sana.


Miongoni mwa dalili za mafua ni pamoja na kuumwa kichwa na homa kidogo, kikohozi au kukereketwa kooni, kuchuruzika kwa kamasi (aina ya majimaji) puani pamoja na uchovu na maumivu ya maungo.

Aidha, njia pekee ya kujikinga na mafua ni kujenga kinga ya mwili kwa kufuata kanuni za afya bora, lakini dawa zote zinazotumika kwa ajili ya kutibu mafua ni kujaribu kumwezesha mgonjwa arudi hali ya kawaida mapema iwezekanavyo. Ndio maana upo usemi kuwa mafua hayana dawa ya moja kwa moja.

Moja ya mbinu ya asili ya kumaliza tatizo la mafua ni pamoja na hii ya kutumia limao, ambapo mhusika anapaswa kutengeneza juisi ya limao moja katika glasi ya maji ya uvuguvugu.


Ongeza kijiko kimoja cha mezani cha asali kisha koroga vizuri na kunywa polepole na uatatakiwa kutumia tiba hii asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu.


Mbali na tiba hiyo ya limao pia bamia, ukwaju, pilipili manga, tangawizi navyo pia ni miongoni mwa tiba nyinginezo za mafua.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment