Thursday, 9 February 2017

Faida za kula kwa mpangilio zipo hapa


Kula kiafya ni moja ya mambo muhimu sana kwa binadamu yoyote kwani husaidia mwili kuwa mbali na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa sugu.

Zifuatazo ni faida ambazo utazipata endapo utaishi kwa kula kiafya:

Kuongeza kipato (uzalishaji mali)
Unapokula kiafya hukusaidia sana kuepuka magonjwa mbalimbali, hivyo kupunguza hata zile safari za kuelekea hospitali mara kwa mara na hivyo muda mwingi utakuwa ukiutumia kuoongeza pato lako la kila siku.

Inaelezwa kuwa kushindwa kula kiafya hukuweka katika hatari ya kupoteza uwezo wako wa uzalishaji mali kwa asilimia 66.

Kula kiafya kutakusaidia kuuweka ubongo wako vizuri na kuwa na uwezo mzuri wa kufikiria mambo.

Kula vizuri kiafya huchangia kukuweka mbali na msongo wa mawazo.Kuna baaadhi ya vyakula unaweza kula na kukusaidia kukuweka vizuri na kujihisi una amani zaidi hata kama ulikuwa umezongwa na mawazo.

Baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa matumizi ya vyakula vyenye vitamini C, Omega 3, magnesium husaida sana kumuweka mwanadamu katika hali ya utulivu na amani ndani ya mwili.

 Vitamin C hupatikana kwenye machungwa na Omega 3 hupatikana kupitia vitoweo kama samaki

Husaidi kuthibiti uzito wako
Siku zote mtu anayekula kiafya huwezi kumkuta amaenenepeana hovyo kwani wengi hula kwa waati na hula vyakula vyenye virutubisho muhimu mwilini tu. Hivyo watu wa namna hii huwa ni ngumu kwao kuwa na uzito mkubwa.

Utaonekana mwenye afya
Tabia ya mtu anayekula kiafya siku zote huonekana mchangamfu na mwenye afya, pia huondokana na hatari ya kukubwa na magonjwa sugu kama vile saratani, kisukari pamoja na magonjwa ya moyo, kwahiyo ni muhimu kula kwa afya ili kuepukana na magonjwa hatari kama hayo.

Utaishi maisha marefu
Unapoishi kwa kula kiafya basi utakuwa na nafasi nziri ya kuishi maisha marefu zaidi ya yule anayekula bia mpangilio. Mfano mzuri tunaupata kwa wazee wetu wazamani wao walikuwa wanakula vyakula vya kawaida kabisa lakini ambavyo ndani yake vilikuwa vimesheheni kila aina ya virutubisho muhimu.

Utaishi ukiwa na furaha zaidi kila siku.
Kile tunachokula ndio huwa matokeo ya akili zetu

Kwa maelezo au ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au dkmandaitz@gmail,com

No comments:

Post a Comment