Saturday, 18 February 2017

Haya ndio matumizi mengine ya parachichi kwa wanaume pekee.


Wanaume wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kutokwa na vipele mara tu baada ya kunyoa ndevu zao.

Mbaya zaidi asilimia kubwa ya wanaume wamekuwa wakishindwa kujua nini cha kufanya ili kuondoa tatizo hilo ambalo pia huharibu muonekanano wa mhusika.

Hapa napenda kukueleza kuwa tunda la parachichi nalo huweza kuondoa tatizo hilo au kupunguza madhara kwa mtu mwenye shida  hiyo.

Jambo la kufanya ni kupata tunda hili fresh kisha limenye na baadaye kulisaga halafu utalitumia mara tu baada ya kunyoa ndevu zako kwa kupaka rojorojo hilo la parachichi sehemu zote za kidevu yaani hii unaweza kuiita 'after shave ya asili'.

Tunda hili la parachichi linauwezo wa kuondoa tatizo hilikutokana na kuwa mafuta mazuri kwa ngozi ambayo pia husaidia kufanya ngozi kuteleza na kuwa laini na yenye afya.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na nyingine nyingi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment