Tuesday, 7 February 2017

Je, unafahamu kuhusu mapindigesi (Peaches) ? Kumbe husaidia kutuliza homa


Mapindigesi au kwa lugha ya kingereza huitwa apricots ni moja ya matunda ambayo hupatikana zaidi mikoa ya nyanda za juu kusini hasa Iringa.

Matunda haya yamesheheni virutubisho kadhaa ikiwa ni pamoja na vitamin za aina mbalimbali.

Leo napenda kukueleza msomaji wangu baadhi ya faida ambazo hupatikana kwa kula matunda haya ya pendigesi.

1. Husaidia kuongeza uoni mzuri.
Hii ni kwa sababu ni tunda lenye vitamin A ya kutosha, lakini pia ndani yake lina vitamin C pia ndani yakke kuna kirutubisho kiitwacho beta - carotene  ambayo humuondoa mhusika kwenye hatari ya kupatwa na tatizo la kuona.

2. Hulinda afya ya mifupa.
Matunda haya pia huimarisha mifupa na kupunguza hata maumivu ya mifupa pia hasa sehemu za maungio, hivyo unapotumia tunda hili mara kwa mara husaidia kuondoakana katika matatizo hayo.

3. Hutuliza homa
Maatumizi ya juisi itokanayo na mapindigesi huwa na nafasi kubwa ya kutuliza homa hasa pale juisi hiyo inapochanganywa na kiasi kidogo cha asali halisi.

4. Ni msaada kwa wenye anemia
Matunda haya ni chanzo kizuri cha madini chuma ambayo husaidia utengenezaji wa damu ndani ya mwili.

5. Huboresha afya ya upumuaji
Matunda haya yanaaminika kuwa na uwezo wa kuwasaidia wale wenye shida ya asthma.

Zingatia: Unapoona hali yako si nzuri ni vyema kufika kwenye kituo cha afya ulichokaribu nacho kwa msaada zaidi.

Kuna mengi zaidi kuhusu tunda hili lakini kwa leo naomba niishie hapa kama unahitaji kujua mengi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com  

No comments:

Post a Comment