Wednesday, 15 February 2017

Jifunze kuacha kusikiliza maneno haya kama unahitaji kufanikiwa kimaisha

Leo napenda kukueleza msomaji wangu kuwa kila unayemuona leo anamafanikio basi tambua alipambana na hakukata tamaa pale alipokutana na vikwazo mbalimbali.

Pia ni vizuri utambue kuwa siku zote kukata tamaa ni adui mkubwa wa mafanikio. Unapojaribu jambo mara moja ukashindwa kisha ukakata tamaa, ni dhahiri hukuwa umedhamiria kufanikiwa katika jambo hilo. Kwani siku zote watu wenye dhamira ya kweli  huwa hawakati tamaa hujaribu tena na tena na tena mpaka pale ambapo wataona ndoto zao zimetimia.

Pamoja na hayo siku zote tambua kuwa katika maisha yako wapo baadhi ya watu wanaokuzunguka ambao hawawezi kufurahi kukuona unakuja kuishi maisha mazuri wao muda wote wanatamani kukuona ukiishi katika maisha duni.

Kutokana na hilo usishangae watu hao wakakupiga vita na wakati mwingine kukukatisha tamaa kwenye yale unayoyafanya. Huenda wakakwambia huwezi kufanikiwa kwa sababu hauna elimu au watakuambia huwezi kwasababu huna mtaji mkubwa nk.

Ukiwa na akili ndogo zisizojua kuchambua mambo, unaweza kuona wanachokisema ni kweli na ukajikuta unapunguza kama siyo kuacha kabisa jitihada za kupambana kutafuta mafanikio yako.

Sasa ili kupambana na hayo yote na ili uweze kufika katika mafanikio au ndoto zako hakikisha unayazingatia haya;-

Jiambie kabisa kwamba kukata tamaa kwako ni mwiko. Kaa mbali na watu wanaokuambia maneno ya kukukatisha tamaa, fahamu hao ni adui wengine katika kufanikiwa kwako.

Kwa maana hiyo usikubali wale waliokata tamaa wakukatishe tamaa, pambana huku ukijua kwamba hakuna wa kuyabadilisha maisha yako isipokuwa ni wewe mwenyewe.

Acha kukukubali ndani ya nafsi yako kwamba umeshindwa na huwezi kufanikiwa, hakuna muujiza utakaojitokeza kutoka mbinguni bali ni juhudi zako.

Kwa leo naomba niishie hapo ila kama unahitaji kuyafahamu mambo haya mengi zaidi hakikisha unahudhuria semina ya ujasiriamali itakayofanyika pale Msimbazi Center siku ya tarehe 25/02/2017 Jumamosi na utajifunza mengi zaidi kutoka kwa Mkufunzi Mtaalam Mandai na wengine wengi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment