Friday, 17 February 2017

Jinsi ya kuvumilia maudhi ya mwenzi mwenye ujauzito

Naimani kuwa baadhi ya watu ambao wapo kwenye ndoa na tayari wanafamilia yaani watoto wanaweza kuwa mashahuda kuhusu hali ya ujauzito na mahusiano jinsi yanavyokuwa.

Wanandoa wenye familia bila shaka wanatambua kuwa hakuna kipindi kigumu katika uhusiano wa kimapenzi kama pale mwenzi wako anaposhika ujauzito.Hii ni kwasababu  wanawake wengi huwa na mabadiliko makubwa ya tabia, jambo ambalo huchangia baadhi ya wanaume washindwe hata kuvumilia.

Sasa basi kwa faida ya wale ambao bado hawajafikia hatua ya kuwa na familia na tayari wapo kwenye mahusiano napenda wajifunze haya machache ambayo huenda yatawasaidia pale wenzi wao watakapofanikiwa kushika ujauzito.

Kwanza tambua kuwa mwanamke mjamzito huenda akawa kila unachokifanya anakiona kibaya, kila kitu kinamkasirisha, muda wote anakuwa na hasira au kisirani kiasi cha kufanya uione nyumba chungu? Kikubwa unapoona hali hiyo usijali, unachopaswa ni kumuelewa na kumsaidia kwani anakuwa katika kipindi kigumu sana kihisia, kiakili na kimwili.

Tambua hakuna kipindi ambacho mwanaume anapaswa kumnyenyekea mwenzi wake kama kipindi hiki cha ujauzito. Kwani safari ya miezi tisa kubeba kiumbe tumboni si mchezo, wanawake wenyewe watakuwa mashahidi kwa jinsi safari ya kulea ujauzito mpaka kujifungua ilivyo ngumu.

Katika kipindi hiki, ni kawaida kabisa kwa mwanamke kuonesha mabadiliko makubwa kama nilivyosema hapo awali, hasa kipindi ambacho mimba inakuwa bado ndogo.

Ni kipindi ambacho anaweza kusema au kufanya jambo lolote bila kujali madhara yake. Kwaani anakuwa siyo yeye, hivyo huhitaji faraja kutoka kwa mume au mwenzi wake ambaye yupo naye karibu kila siku.

Wapo baadhi ya wanawake wakibeba ujauzito, huwachukia waume zao kupitiliza na hata kutolala nao kabisa.

Hata hivyo, kumbuka kuwa pamoja na hayo yote haina maana kwamba mapenzi yameisha, la hasha hicho ni kipindi cha mpito tu. Hivyo hakuna sababu ya kukasirika hata kama atakuwa anakuudhi na kukukasirisha kiasi gani.

Hapa chini nimekuwekea video ya Tunda Man Mama Kija ambayo naamini itasindikiza ujumbe huu vizuri. Karibu tuitazame hapa chini>>>


Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment