Saturday, 11 February 2017

Kabla ya kuoa kijana jifunze hizi tabia 9 za wanawake hapa

Waswahili husema bora ukosee kujenga kuliko kukosea kuoa na ndio maana na mimi nimeona leo nikwambie sifa hizi za wanawake ambazo zinaweza kukusaidia wewe kijana ambaye bado hujaoa.

Zifuatazo ni sifa za wanawake mbalimbali:-

MWANAMKE MWENYE HOFU YA KUSALITIWA
Huwa ni mwaminifu alishawahi kusalitiwa au aliwahi kushuhudia watu wakisalitiwa, hupenda kukagua simu ya mwanaume mara kwa mara na wakati mwingine hata kudhubutu kunusa za mwanaume wake kabla ya kuzifua. Hivyo kama unatabia ya kuchepuka aina hii ya wanawake haitakufaa.

MAMA WATOTO
Wanawake wa aina hii huwa ni adimu na wachache hivyo ni wanaume wachache ambao hubahatika kuwapata. Sifa za wanawake wa aina hii ni wakarimu, sio wabinafsi na hupenda kumjali mwanaume na kumtimizia mahitaji yote anayopaswa kupewa na anaheshima na kujiheshimu. Hivyo wewe kama mwanaume unayehitaji mke ukikutana na mwanamke wa aina hii weka ndani.

MWANAMKE MKOROFI
Hufanya kile unachomkataza na hufanya tena na tena, mara nyingi huwa haridhiki hata umfanyie nini na huwa na tabia ya kulalamika hovyo. Pia huweza hata kumkalipia mwanaume wake yaani kwa kifupi raha yake ni kuona mwanamke anakasilika.

MWANAMKE MBANA MATUMIZI
Huwa hapendi kuishi maisha ya kifahari hata akiwa na pesa kiasi gani basi yeye huendelea kuishi maisha yake ya kawaida. Pia si mtu wa mavazi sana na huwa na nguo chache tu na nimuongeaji sana

MWANAMKE PASUA KICHWA
Huyu hutoka kimapenzi na watu wengi kwa nyakati tofauti na anamvuto pia hupenda kuvaa nguo fupi za kubana zinazo onesha maungo yake kama mapaja nk. Yeye kwake kukuacha wala si jambo la ajabu ni kawaida kabisa na yeye ukimuacha huwa haoni shida kabisa.

MWANAMKE MLIZI
Huyu yeye kila kitu hulia hata kama ni jambo dogo basi atatoa machozi. Mfano mwanaume ukichelewa kurudi kidogo tu utamkuta sebuleni analia kisa alikuwa hajui uliko. Huyu hufaa kuolewa lakini na mtu mwenye mapenzi ya kweli.

MWANAMKE WA KUIGA

Huyu anapenda sana kumiliki vitu kama wanavyomiliki rafiki zake hata kama hana uwezo navyo. Pia ni mwepesi wa kusikiliza maneno ya pembeni na kuyaamini.

MWANAMKE MWENYE HOFU YA MUNGU
Hupenda kufanya ibada kanisani/ msikitini si mtumiaji wa vitu vya anasa kama pombe, sigara nk. Hufanya mambo mazuri yanayokubalika katika jamii. Hupenda wanaume wenye kuvaa mavazi ya heshima na wenye lugha nzuri.

MWANAMKE WA SHUGHULI
Huyu hawezi kukubali kupitwa na sherehe yoyote iwe kitchen party, kigodoro, disko n.k na mara nyingi hubadilika baada ya umri kusogea sana 

Kiukweli zipo sifa nyingi za wanawake lakini hatuwezi kuzimaliza kwa mara moja leo naishia hapa naomba endelea kufuatailia tovuti hii ili kujifunza mengi zaidi au wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment