Wednesday, 8 February 2017

Karafuu, Chumvi, jinsi vinavyoweza kukata harufu mbaya ya miguu haraka

Miguu kutoa harufu mbaya ni moja ya matatizo ambayo huwasumbua watu wengi hususani wanaume wengi katika jamii.

Tatizo hili mara nyingi huwakwaza zaidi wale ambao huishi karibu na watu wenye shida hiyo kutokana na kuwa watu wengi wenye tatizo hili huwa wagumu kukubaliana na hali yao.

Zipo sababu kadhaa ambazo huelezwa kuchangia tatizo hilo, lakini sababu kubwa zaidi ni uchafu  na  ndiyo chanzo kikuu cha miguu kutoa harufu.

Kwa kiasi kikubwa uchafu huo ndio unasababisha kuzaliwa kwa vijidudu vinavyoleta harufu mbaya kwenye miguu.

Licha ya kuwepo kwa tiba mbalimbali ambazo mtu mwenye tatizo hili anaweza kutumia, lakini tiba kubwa zaidi ni ile ya usafi ni jambo kubwa analopaswa kuzingatia mtu mwenye tatizo hili.

Unashauriwa kuwa uwapo na tatizo hili unapaswa kuzingatia kusafisha miguu yako mara kwa mara na ukiiacha mikavu muda wote ili kuepusha unyevunyevu.

Pia unapovaa viatu vya kufunika hakikisha unavaa soksi safi na kavu na uepuka kurudia soksi au kuvaa ambazo hazijakauka vizuri kwani zinaweza kusababisha miguu kunuka mara dufu.

Usivae viatu vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili vikauke na kupunguza uwezekano wa kutokea harufu.

Kama utahisi tatizo ni kubwa unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 ili tukupatie njia nyingine za asili za kumaliza shida hiyo. Ikiwa ni pamoja na kutumia chumvi, karafuu, baking soda.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment