Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 20 February 2017

Kila kitu huwa na faida na hasara yake !! hii ndio hasara ya kula parachichi

Is Avocado Bad for Your Health?
Mara nyingi tumekuwa tukizungumza kuhusu umuhimu wa vyakula mbalimbali pamoja na ulaji wa matunda likiwemo tunda la parachichi.

Parachichi ni miongoni mwa matunda yenye faida lukuki naamini kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii bila shaka utakuwa unafahamu baadhi ya manufaa ya tunda hili, lakini leo napenda tuelezane moja ya athari ambazo huweza kujitokeza endapo utakula tunda hilo kupita kiasi.

Tukumbuke kuwa wahenga husema kila chenye faida basi huweza kuwa na madhara yake pia, sasa moja ya madhara ya parachichi ni pamoja na kusababisha mlaji kuongeza uzito wa mwili 'unene'.

Hivyo kama wewe huhitaji kabisa kuwa mnene au kuwa na uzito mkubwa basi unashauriwa kutotumia tunda hili mara kwa mara ili kuweza kuepuka hali hiyo.

Zingatia: Si kwamba tunda hili ni baya hapana, hili ni tunda nzuri hasa kiafya kutokana na kuwa na virutubisho mbalimbali na muhimu ndani ya miili yetu, lakini unapolitumia kupita kiasi ndio huweza kuleta madhara hayo nakujikuta unanenepa sana.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment