Wednesday, 1 February 2017

Kitunguu swaumu kinavyoweza kumaliza kichomi ndani ya dakika kadhaa tu!


Kitunguu swaumu ni moja ya viungo ambavyo hutumika kwenye mapishi mbalimbali katika kuongeza ladha ya chakula, lakini pia kiungo hiki kinasifika kwa kuwa na manufaa mbalimbali ikiwa kitatumika vyema.

Mara kadhaa tumekuwa tukielezana kuhusu faida za kiungo hiki kupitia mtandao wetu huu, lakini leo tena nahitaji kukueleza kuhusu namna kiungo hiki kinavyoweza kupunguza maumivu ya kichomi.

Namna ya kutumia
Ponda punje kumi za kitunguu swaumu hadi ziwe katika hali ya uji uji kisha paka sehemu za kifua zenye maumivu huku ukichua kwa utaratibu sana. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment