Thursday, 2 February 2017

Magome ya ukwaju yanavyoweza kusaidia afya ya uzazi kwa wanawake


UKWAJU kwa kawaida huwa na ladha fulani hivi ya uchachu, lakini pia ni moja ya kiburudishio kizuri ambacho kimesheheni virutubisho kadhaa.

Bila shaka wengi hutumia tunda hili lenye ladha ya ugwadu (uchachu) kwa kutengeneza juisi ambayo hutumika kama kinywaji kinachoburudisha.

Hata hivyo, ukwaju unaelezwa kuwa na faida nyingi kwa binadam tofauti na watu wengi wanavyofahamu, lakini leo tutaangazia faida za magome ya ukwaju.

Gome la ukwaju likianikwa kivulini kwa siku kadhaa na kisha kutwangwa na ukapatikana unga wake hiyo husaidia sana wanawake ambao hukubwa na kifafa wakati wa uzazi.

Pia gome hilo la ukwaju linauwezo wa kuwasaidia wanawake wenye shida ya kujifungua watoto wafu mara kwa mara, lakini pia huweza kuwasaidia wanawake wenye tatizo la kubeba mimba na kutoka kabla ya wakati wa kujifungua.

Namna ya kuandaa tiba hii chuna gome la mkwaju na uanike kivulini baada ya kukauka litwange vizuri, lakini kumbuka kuwa haya ni masuala yanayowahusu wanawake hivyo ni vizuri dawa hii ikaandaliwa na mwanamke tena aliyekwisha koma hedhi.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment