Friday, 3 February 2017

Mambo matatu ya kufanya uwapo ofisini ili uendelee kuwa na afya bora


Watu wengi wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku hujikuta wakizingatia zaidi kazi na hata kusahau umuhimu wa afya zao.

Hapa nakuletea mambo kadhaa ambayo ni muhimu kuyazingatia uwapo ofisini unaendelea na kazi zako.

1. Kwanza hakikisha kiti unachokalia kinaruhusu mgongo wako kukaa vizuri bila kuinama wakati wote wa kazi na miguu inafika chini na kugusa sakafu, hii itakusaidia kuepuka matatizo ya mgongo kwa baadaye na miguu pia.

2. Kuwa na muda wa mfupi mfupi wa mapumziko, kwani kufanya kazi kutwa nzima pia si vizuri kiafya na baada ya siku kadhaa utajikuta utendaji wako unapungua zaidi na kuanza kulipua kazi zako, hivyo kumbuka kuwa mapumziko ni muhimu na utakapopumzika unaipatia akili yako nguvu mpya ya kufikiri na kufanya kazi vizuri ziidi.

3. Jitengenezee utaratibu wa kunywa maji mara kwa mara wakati unapoendelea na kazi zako ofisini angalau kunywa lita mbili hadi tatu kwa siku tangu unapoingia ofisini kwako. Ili ufanikiwe katika hili itakubidi kuwa na chupa na glasi yako ya maji mezani kwako ambapo utakuwa ukiiona mara kwa mara.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment