Saturday, 18 February 2017

Namna ya kutumia majani ya mpera katika kuboresha afya ya nywele zako


Ni ngumu kuamini kuwa majani ya mpera yanaweza kuwa sehemu ya bidhaa inayoweza kubadili muonekano wako mwanamke na kukufanya kuonekana mrembo zaidi hususani katika upande wa nywele zako.

Hi ni kutokana na majani hayo kuwa na uwezo wa kuzilinda nywele zako kutokatika hovyo na kuzifanya kukua vizuri na kuendelea kuonekana na afya bora.

Nimeona nikuletee hii kwani naamini inaweza kuwasaidia wale wasio na uwezo wa kwenda saloon kila wiki, hivyo wataweza kutumia mbinu hii asili kuendelea kuboresha afya nywele zao.

Jambo la kufanya ni kupata majani hayo ya mpera kiasi cha fungu moja kama la mboga ya majani kisha chemsha kwa muda usiopungua dakika 15 hivi na uyaache yapoe.

Baada ya hatua hiyo chukua maji ya hayo yachuje kisha ubaki na maji ya mpera tu bila majani yake na uanze kutumia maji hayo kuoshe nywele zako, huku ukihakikisha yanafika hadi kwenye mzizi wa nywele zako.

Baada ya hapo acha kwa dakika kadhaa kisha utaosha nywele zako na baadaye kupaka mafuta yako unayotumia, yanaweza kuwa ya nazi ili kupata matokeo mazuri. Kumbuka kuwa maji ya majani hayo ya mpera pia husaidia kuondoa hata tatizo la mba kwenye nywele.

Fanya zoezi hilo mara kwa mara bila shaka baada ya muda fulani utaanza kujionea mabadiliko ya afya za nywele zako.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment