Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 21 February 2017

Njia 3 asili za kulinda afya ya figo yakoFigo ni moja ya kiungo muhimu ndani ya mwili wa binadamu, kwasababu kiungo hicho kina ushirikiano wa karibu pia na moyo hivyo kuathirika kwa figo huweza kuchangia athari kwenye mfumo wa damu na mapigo ya moyo.

Kazi kubwa ya figo mwilini ni kuchuja taka mwili zilizomo na kuzitoa nje kwa njia ya mkojo pamoja na kupunguza kiasi cha maji kilichozidi mwilini.

Aidha, figo pia hufanya kazi ya kufyonza na kuvirudisha vitu muhimu ambavyo vingehitajika kutoka kwa njia ya mkojo, lakini pia figo husaidia kudhibiti madini kama vile potassium, magnesium ambayo ni muhimu ndani ya mwili, hivyo basi figo inapopoteza uwezo wake wa kufanya shughuli zake huweza kuchangia  kukosekana kwa ufanisi wa shughuli nyingine ndani ya mwili.

Zipo hapa njia asili ambazo huweza kusaidia kuboresha afya ya figo yako:-

1. Kunywa maji mengi

2. Kudhibiti matumizi ya chumvi

3. Punguza au acha matumizi ya pombe

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment