Saturday, 11 February 2017

Sababu 6 zinazochangia mimba kuharibika


Baadhi ya wanawake wamekuwa wakiuliza maswali kuhusu sababu ambazo huchangia mimba kuharibika mara kwa mara.

Leo nimeona nizitaje hapa sababu ambazo huweza kuchangia mimba kuharibika:-

1.Umri.
Wanawake wenye umri mkubwa huweza kuwa na hatari ya mimba kuharibika pale wanaposhika mimba. Umri huo ni kuanzia miaka 40 na tauendelea, licha ya kwamba si lazima kila  mwanamke mwenye umri huo kukumbwa na tatizo hilo.

2. Wanawake wenye historia ya tatizo hilo.

3. Magonjwa
Magonjwa nayo ni moja ya sababu za tatizo hilo, mfano wa magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya zinaa n.k

4. Ufutaji wa sigara na matumizi holela  ya dawa bila kupata ushauri kutoka kwa wataalam wa afya.

5. Sababu za kimazingira
Mfano kuishi karibu na sehemu zenye asili ya hewa yenye kemikali huenda kutokana na viwanda kadhaa.

6. Uzito mkubwa
Zipo tafiti kadhaa ambazo zinaonesha kuwa uzito mkubwa huweza kuchangia mimba kuharibika wakati kadhaa.

Hata hivyo zipo dalili ambazo huashiria mimba kuharibika ikiwa ni pamoja na kuhisi maumivu makali chini ya tumbo pamoja na matone ya damu kuanza kutoka sehemu za siri, Hivyo uonapo dalili hizo ni vyema ukafika mara moja kwenye  kituo cha afya kwa msaada zaidi.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment