Tuesday, 7 February 2017

Sababu zitakazokufanya uanze kula samaki zaidi kuliko kitoweo kingine


Watu wengi ni walaji wasamaki, lakini si kila mlaji wa samaki anatambua umuhimu wa kitoweo hicho kiafya na kilivyo na umuhimu mkubwa ndani ya miili yetu.

Hapa ninazo faida kadhaa za matumizi ya kitoweo cha samaki

Kwanza kabisa itambulike kuwa kitoweo hiki pekee ndio kinatajwa kuwa na mafuta yenye kiambata cha Omega 3 ambayo huelezwa kuwa na manufaa mengi mwilini ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezo wa kufikiri pamoja na utunzaji kumbukumbu.

Faida nyingine za kitoweo hicho ni pamoja na kuongeza uoni mzuri na kumsaidia mtumiaji kupata usingizi mzuri usiokuwa na bugudha, lakini pia ni kitoweo ambacho kinaelezwa kusaidia kwa wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito (mwili).

Pamoja na hayo kitoweo hicho kinatajwa kuwa na umuhimu katika ulinzi wa afya ya moyo kwa ujumla wake, hivyo ni vyema kukitumia mara kwa mara kwaajili ya kulinda afya ya kiungo hicho muhimu ndani ya mwili.

Kwa ushauri zaidi unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment