Thursday, 16 February 2017

Ukikubali kuacha tabia hizi 5 lazima ufanikiwe katika maisha yako


Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakishindwa kufanikiwa katika maisha yao kutokana na vijisababu fulani fulani.

Siku zote kama unahitaji mafanikio ya kweli lazima ukubali kuacha aina fulani fulani za tabia ili kuzivikia ndoto zako.

Miongoni mwa mambo muhimu ambayo huweza kukusaidia kufanikiwa katika maisha ni pamoja na kuachana na tabia hizi au mawazo haya yafuatayo:-

1. Acha kupenda kuhairisha mambo mara kwa mara bila kuwa na sababu za msingi sana. Kama umeamua kufanya basi hakikisha unajipanga na kufanya kweli.

2. Acha kukata tamaa, ukiendekeza tabii basi tarajia kushindwa kila siku katika maisha yako au mipango yako. Jitahidi kuamini kuwa unaweza na kamwe wewe si mtu wa kushindwa.

3.Punguza visingizio, jenga utamaduni wa kuacha kusingizia vitu fulani hasa pale unaposhindwa kwani unapoogopa kusingizia pia utaogopa kushindwa.

4. Acha matumizi ya hovyo ya fedha, jitahidi kuiheshimu pesa pale unapoipata kila unapohitaji kuitumia kumbuka namna ulivyoihangaikia kuipata ukikumbuka hivyo lazima utaiheshimu pesa  yako na kuipa thamani.

5.Acha uvivu, hii tabia ni mbaya na imewafanya wengi kushindwa katika maisha yao, hivyo hakikisha unaepukana nayo ikiwa unapenda kufikia mafanikio au ndoto zako.

Kwa masomo mengine kama haya ikiwa ni pamoja na uandaaji bidhaa mbalimbali kama vile mkate, keki, tomato sauc na tomato paste hakikisha tunakutana siku ya tarehe 25/02/2017 pale Msimbazi Center Ilala jijini Dar es Salaam ambapo Mkufunzi Mandai na wengine wengi watakueleza mambo mengi kuhusu kufanikiwa kwako.

Pia unaweza kutupigia simu kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment