Tuesday, 14 February 2017

Ukiona dalili hizi jua unatatizo kiafya

Kwa kawaida sisi miili yetu binadamu huonesha dalili fulani endapo kuna tatizo ndani ya mwili, lakini kwa bahati mbaya sana watu wengi hawana uelewa wa dalili hizo.

Leo naomba nikueleze hizi dalili chache ambazo huashiria uwepo wa tatizo ndani ya mwili.

Midomo kuwa mikavu
Midomo ni sehemu tosha ya kuashiria tatizo ndani ya mwili na mara nyingi huweza kuashiria kupungua kwa kiwango cha maji mwilini. Kwani unapokosa maji ya kutosha mwilini basi hata midomo nayo huanza kupoteza unyevunyevu. Hivyo kwa wale wakinadada ambao hulazimika kulainisha midomo yao kwa 'lips shine' basi watambue kuwa wana upungufu wa maji mwilini.

Ili kukabiliana na tatizo hili unapaswa kuanza kunywa maji ya kutosha zaidi ilivyo sasa angalau glasi 8 kwa siku

Kufunga choo
Hii huwa ni dalili ya wazi  kuwa mhusika anashida ya ukosefu wa kamba lishe (fibre) mwilini. Kwa kawaida binadamu anatakiwa kupata choo kikubwa kila siku kilicho laini na kingi. Iwapo hupati choo kila siku na ukipata unapata kigumu, tena kidogo, jua una matatizo!

Haja kubwa ni muhimu kwa sababu ndiyo inayosafisha tumbo, uchafu unapokaa tumboni kwa muda mrefu, sumu zilizomo kwenye haja kubwa hurejea mwilini na kusababisha madhara mengi ya kiafya.

Vidonda vya mdomo
Vidonda vya midomoni, huwa ni dalili moja wapo ya dalili za upungufu wa vitamini B mwilini na mara nyingi huwatokea wale wapenzi wa  kula vyakula vya kwenye makopo (processed foods) na kula sukari kwa wingi.

Njia pekee ya kuondokana na tatizo hili ni kuanza kula vyakula vyenye kuongeza vitamin B kwa wingi. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kingi cha vitamin B ni pamoja na  viazi vitamu na nafaka isiyokobolewa nk.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment