Wednesday, 15 February 2017

Aina 4 ya vyakula vinavyoshauriwa kuliwa na wagonjwa wa moyo

Unaambiwa kuwa uzuri wa tatizo ni pale unapolijua kuliko kutolijua na siku zote hakuna jambo jema kama mtu mwenye matatizo ya kiafya kujua ni aina gani ya mlo anaopaswa kula au kutokula.

Baadhi ya magonjwa kama vile ‘presha’, vidonda vya tumbo, magonjwa ya moyo, n.k, mara nyingi huhitaji kubadili hata mtindo wa maisha hususani mlo pia.

Leo tutaangalia baadhi ya vyakula na matunda anavyopaswa kula mtu mwenye ugonjwa wa moyo, ambavyo huweza ama kudhibiti hali yake isiendelee kuwa mbaya.

Asali
Asali ina virutubisho ambavyo vina uwezo wa kuzuia aina zote za matatizo ya moyo. Inaelezwa kwamba asali inaboresha mzunguko wa damu mwilini, halikadhalika inaondoa matatizo mengine ya moyo. Kijiko kimoja (cha chakula) cha asali kikitumiwa kila siku mara baada ya mlo, kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya maradhi yote ya mwili.

Apple

Tunda hili husaidia kwa mgonjwa wa moyo, hasa wenye matatizo ya kuwa na moyo dhaifu, hivyo wale wenye matatizo hayo wanashauriwa kupendelea kula apple mara kwa mara, ikiwemo juisi yake ambayo huweza kuleta matokeo mazuri zaidi.

Zabibu

Zabibu ni tunda linaloongoza kwa ubora linapokuja suala la kuimarisha afya ya moyo. Ili kupata matokeo mazuri, andaa ratiba maalum ya kula zabibu peke yake kwa siku kadhaa mfululizo, juisi ya zabibu pia hufaa zaidi.

Kitunguu
Kitunguu kina faida kubwa kwa mgonjwa wa moyo,  kwakuwa huweza kurekebisha mafuta ya kolestro ndani ya mwilini na kuuweka mwili katika hali yake ya kawaida. Kwa matokeo mazuri, kunywa kijiko kimoja (cha chakula) cha juisi ya kitunguu.

Pamoja na hayo, matunda na mbogamboga kwa ujumla wake, ndiyo vyakula muhimu kwa magonjwa mengi ya moyo, vyakula hivyo vina uwezo wa kudhibiti ugonjwa huo na kuimarisha moyo.

Sambamba na hayo, watu wenye matatizo ya moyo hushauriwa kuepuka matumizi ya chumvi nyingi, kahawa, sukari, sigara nk. Hayo yakizingatiwa, mgonjwa anaweza kuishi na tatizo la moyo bila kusumbuliwa.

Zingatia. Kama utakuwa na matatizo haya ya moyo ni muhimu kufika kwenye kituo cha afya au hospitali iliyokaribu nawe ili uweze kupatiwa msaada zaidi

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment