Saturday, 4 February 2017

Vitu vitano ambavyo havitakiwi kukosekana jikoni kwako kila siku

Top Ten Foods Everyone Should Have In Their Kitchen At All Times!
Unapokuwa na familia kama mzazi hasa mama unatakiwa kuhakikisha familia yako muda wote inapata vyakula vyenye virutubisho na kujenga mwili ndani yao.

Hivyo basi kwa kulitambua hilo leo nimeona nikuletee hivi vitu muhimu ambavyo kama Mungu atakuwa amekujalia uwezo basi utapaswa kujitahidi muda wote viwe vinapatikana jikoni kwako.

1. Spinach.
Hii ni mboga ya majani ambayo ni muhimu kuwepo jikoni kwako muda wote kutokana na uwezo wake wa kusaidia wa kusawazisha kiwango cha sukari mwilini na kulinda ngozi, mifupa.

2. Machungwa.
Hakikisha muda wote tunda hili linapatikana ndani mwako (jikoni) kutokana na kuwa na vitamin C ya kutosha na kusifika kwake kwa kuimarisha kinga za mwili pia.

3. Kitunguu
Ni kiungo muhimu pia jikoni, lakini pia husaidia kulinda afya ya moyo kwa mujibu wa wataalam .

4. Nyanya
Huhitajika sana jikoni katika kukamirisha mapishi lakini pia inaelezwa kuwa na uwezo wa kupunguza uwezekano wa saratani ya kibofu kwa wanaume. Pia imesheheni vitamin C.

5. Tangawizi
Ni kiungo ambacho pia huhitajika sana jikoni na pia husifika kwa kuwa na uwezo wa kupunguza maumivu ya tumbo na maumivu ya viungo 'joint'.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment