Wednesday, 8 February 2017

Viungo ambavyo husaidia kutuliza majeraha ya kukatwa na chupa au wembe kwa haraka


Je, ni mara ngapi umewahi kujikata na chupa? au mtoto wako wakati akicheza bahati mbaya akajikuta amekatwa na chupa, je nini ulifanya kumsaidia?

Sasa basi leo nataka kukueleza baaadhi ya mambo ya kufanya endapo utakatwa na chupa ikiwa kama huduma ya kwanza.

1. Kitunguu saumu
Kwanza utachukua kitunguu swaumu na kukisaga kisha changanya na asali kidogo halafu tumia mchanganyiko huo kupaka sehemu ya jeraha lililotokana na kujikata na chupa. Kisha baada ya dakika 5 au 10 ondoa mchanganyiko huo kwenye jeraha na kunawa na maji ya uvuguvugu sehemu ya jeraha.

Fanya zoezi hilo angalau mara mbili kwa siku na utaona matokeo mazuri pasipo shida yoyote.

2. Alovera
Andaa mualovera kisha kata na kupata maji yake halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka sehemu yenye jeraha na utaona matokeo mazuri mara tu baada ya kutumia mualovera huo.

3. Asali
Nayo ni njia nzuri na bora ya kumaliza tatizo kujika kwa na chupa.

Baada ya kuzifahamu njia hizo lakini kumbuka kuwa unashauriwa kufika kwenye kituo cha afya kwa msaada zaidi unapoona jeraha bado linaendela kutoa damu.

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment