Saturday, 18 February 2017

Zifahamu hizi dalili 5 za hatari kwa mama mjamzito

Wakati wa kipindi cha ujauzito ni moja ya vipindi vizuri na muhimu kwa mama pamoja na familia nzima kwa ujumla.

Pamoja na uzuri wa kipindi hiki, lakini pia ndio kipindi ambacho mama huweza kupata shida mbalimbali ambazo husababishwa na mabadiliko ndani ya mwili wake.

Hivyo katika kipindi hiki ni lazima mama kuwa makini sana na kuwa karibu na kituo cha afya pamoja na wataalam wa afya pia. Kwani hiki ndio kipindi ambacho  kuna mambo ambayo mama anapoyasikia mwilini mwake ni lazima atoe taarifa kwa watu wake wakaribu mara moja ikiwa ni pamoja na kufika kituo cha afya.

Baadhi ya mambo muhimu ambayo mama hupaswa kuripoti haraka kila anapohisi hali hizo ni pamoja na haya yafuatayo hapa chini:-

1. Kutokwa na damu sehemu za siri.

2. Kuhisi hali ya mtoto kutocheza tumboni

3. Maumivu makali ya tumbo & kichwa

4. Kuuma au kuvimba kwa miguu

5.Kuhisi kupatwa na uchungu kabla ya wakati.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na nyingine nyingi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment