Tuesday, 21 March 2017

Aina 3 ya vinywaji muhimu kwa mama mjamzito


Wakati wa ujauzito ni moja wa nyakati ambazo mama huhitaji ukaribu sana na kuzingatia taratibu zote za mlo.

Pia wakati huo mama huhitaji kuzingatia kunywa maji ya kutosha na vinywaji mbalimbali.

Vifuatavyo ni vinjwaji muhimu ambavyo huhitajika wakati wa ujauzito kwa kinamama.

1. Juisi ya mbogamboga
Juisi hii ya mbogamboga inaweza kuwa ni mchanganyiko wa spinach, karoti ambayo hufaa kwa mamamjamzito.

2. Juisi ya matunda mchanganyiko
Unaweza kuandaa matunda ambayo unayapenda na ukaamua kuyachanganya kwa wakati mmoja na kupata juisi ya aina moja ambayo itakuwa ni nzuri kwa mamamjamzito.Inashauriwa mchanganyiko huo usizidi angalau aina nne za matunda.

3. Maji ya nazi
Maji haya nayo si vibaya mama mjamzito akayapata angalau mara mbili kwa wiki kwa manufaa ya afya ya mama

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment