Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 11 March 2017

Fahamu kuhusu faida za mafuta ya mbegu za tikitimaji

Mara kadhaa tumeshazungumza kuhusu faida za tunda la tikitimaji, lakini leo naomba tuzungumze kuhusu faida za mafuta ya mbegu za tikitimaji.

Miongoni mwa faida za mafuta yatokanayo na mbegu za tikitimaji ni pamoja na kuboresha afya ya ngozi hususani ngozi yenye mafuta mengi.

Mafuta ya mbegu za tikitimaji ni mazuri sana kwa afya ya nywele pia kwani husaidia nywele kukua vizuri na kuwa na afya, lakini pia husaidia kuzuia nywele kukatika.

Husaidia ngozi kutozeeka haraka, matumizi ya mafuta ya mbegu za tikitimaji husaidia kulinda seli za kwenye ngozi na hivyo kumfanya mhusika kutozeeka mapema ikiwa atatumia mafuta haya mara kwa mara.

Ndani ya mafuta ya mbegu za tikitimaji pia kuna vitamin E ambayo husaidia kuimarisha kinga za mwili.

Hizo ni miongoni kati ya faida nyingi za tikitimaji, lakini kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment