Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 10 March 2017

Hatua 3 za kufanya ili kupata kitu ambacho hujawahi kukipata ktk maisha yako


Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wakati mwaka huu 2017 unaanza uliahidi kuhakikisha unatimiza jambo fulani katika maisha yako ambalo hukuwahi kulifanya hata mara moja basi mada hii inaweza kuwa inakuhusu kwa leo.

Napenda kukwambia haya mambo kadhaa ya msingi ambayo unatakiwa kuyafuata endapo unahitaji kupata vitu ambavyo hukuwa kupata katika maisha yako yote.

1. Kwanza unachotakiwa kukifahamu ni kwamba ili ufanikiwe kupata kitu ambacho hukuwahi kukipata katika maisha yako basi tambua kuwa utalazimika kufanya maamuzi ambayo hukuwa kuyafanya katika maisha yako yote na yanaweza kuwa ni magumu zaidi kwako kwasababu ni kitu kipya.

2. Pia itakulazimu kuchukua hatua ambazo hukuwahi kuzifanya katika maisha yako yote tangu uzaliwe nazo pia huweza kuwa ngumu lakini yakupasa uzishinde.

3. Hatua ya tatu itakulazimu kuelekea muelekeo ambao hukuwahi uelekea katika maisha yako yote lakini katika wakati huo itakubidi uelekee hivyo ili kufanikiwa.

Hivyo kumbuka kuwa unapohitaji kuingia labda kwenye biashara fulani au kazi fulani ambayo hujawahi kuifanya hata mara moja basi tambua kuwa utatakiwa kuwa na maamuzi na hatua na muelekeo wa tofauti kabisa katika maisha yako na itakupasa uendane nayo ili kufika salama uendako.

Kwa ushauri zaidi usisite kutupigia simu kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800  au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Kumbuka tupo kwa ajili yako msomaji wetu.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment