Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 8 March 2017

Je, umewahi kusikia kuhusu kiazi hewa 'Air Potato,' zipate faida zake 5 hapa


Kiazi hewa au kwa lugha ya kingereza huitwa air potatoes ni moja ya kiazi cha asili ambaccho ni aghalabu sana kukipata.

Kazi hiki kinaelezwa kuwa na faida mbalimbali za kiafya endapo utaweza kukipata na kukitumia inavyofaa.

Zifuatazo ni miongoni mwa faida za kiazi hewa au 'air potatoes' kiafya:-

1. Kwanza kiazi hiki kinasifika kwa kuwa na uwezo wa kusaidia matatizo ya mbalimbali ya kinamama ikiwa ni pamoja na matatizo ya uzazi endapo kitatumiwa inavyopaswa au kwa kufuata utaalam wa wataalam wa mimea tiba.

2. Pia kiazi hiki huweza kupunguza athari za matatizo ya kuhara.

3.Kwa wale wenye shida ya goita pia wanashauriwa kutumia kiazi hiki kwani huwa na nafasi yake pia katika kutoa ahueni kwa matatizo hayo.

4. Aidha, kiazi hewa pia kinaelezwa kuwa na uwezo wa kupunguza madhara ya matatizo ya upumuaji likiwemo tatizo la pumu.

5. Kiazi hiki pia kinaweza kuwa na manufaa kwa wazee kwani kinauwezo wa kupunguza maumivu ya misuli na mifupa ambalo ni moja ya tatizo linalowakabili wazee wengi.

ZINGATIA
Kila kitu huwa na faida na hasara zake hivyo basi zifuatazo ni baadhi ya  hasara za kiazi hewa au air potatoes.

1. Kwanza hakitakiwi kutumiwa na kinamama wajawazito na wanaonyonyesha.

2. Si kizuri kwa watu wenye vidonda vya tumbo.

3. Huweza kumsababishia mhusika yaani aliyekula kutapika au kuhisi uchovu.

4.Huweza kusababisha madhara ya ini pia.

Kama utahitaji kutumia aina hii ya kiazi ni vyema kuwasiliana nasi kabla kwa ushauri mzuri zaidi kutoka kwa Mtaalam Abdallah Mandai kutoka Mandai Products Company Limited iliyopo Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. 

No comments:

Post a Comment