Friday, 10 March 2017

Je, umewahi kusikia kuhusu kiazi kikuu, zipo faida zake hapa


Kiazi kikuu sio maarufu sana kwa miongoni mwa watu wengi katika jamii, lakini umaarufu wake pengine unaweza ukaanza kuuona leo baada ya kusoma maelezo haya mafupi kutoka kwa Mtaalam Mandai

Kiazi kikuu ni miongoni mwa vyakula vinavyosaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini, matatizo ya hedhi na kuweka sawa mfumo wa homoni za uzazi kwa mwanamke.

Aidha, kiazi hiki kimesheheni virutubisho kadhaa kama vile protini, wanga, sukari na kamba lishe. Pia vitamini vya thiamini, riboflavini, niazini na folate.

Virutubisho vingine kwenye kiazi kikuu ni madini ya magnesiamu, calcium, chuma,potassium , zinc ambavyo kuwapo kwake mwilini husaidia kupambana na maradhi mbalimbali.

Pamoja na hayo, kiazi hicho pia husaidia kuongeza kinga ya mwili na kuupatia mwili nguvu na kusaidia kuondoa matatizo ya uvimbe mwilini pamoja na mifupa.

Jinsi ya kukitumia kiazi kikuu
Andaa kiazi hicho kwa kukikatakata vipande vidogo vidogo na kuvichemsha kwa muda wa dakika zisizopungua 15 hadi 30, kisha kula na inashauriwa kula mlo huo mara kwa mara.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment