Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 16 March 2017

Je, unajua matumizi ya mchanganyiko wa asali na maziwa kwa afya yako? soma hapa


Katika maisha yetu binadamu tunavyoishi kila siku zinavyozidi kwenda basi kwa kawaida mabadiliko hujitokeza ndani ya miili yetu moja ya mabadiliko ni pamoja na ngozi pia.

Ambapo watu wengi umri unaposogea basi hata ngozi nayo huanzakutengeneza mikunjo hasa mikononi na shingoni pia.

Leo hapa ninayo mbinu itakayokusaidia kuondosha mikunjo mwilini mwako. Karibu twende sote hapa.

Matumizi ya maziwa na asali yanatosha kabisa kuondosha tatizo hilo ikiwa utafanya haya yafuatayo:

Kwanza kabisa kwa kawaida maziwa na asali vyote kwa pamoja ni bidhaa muhimu kwa afya ya ngozi zetu.

Maziwa huwa na masaada mkubwa wa kuondosha madoa mwilini, lakini asali yenyewe msaada wake ni katika kuhakikisha inaifanya ngozi inabaki kuwa na unyevunyevu wakati wote.

Namna ya kuandaa asali na maziwa ili ya kusaidie kuondosha mikunjo inabidi upate nusu kikombe cha maziwa pamoja na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja cha sukari.

Baada ya kuvipata vyote hivyo utachanganya kwa pamoja kisha tumia kwa kupata sehemu zenye mikunjo mwilini mwako kisha acha mchanganyiko huo mwilini mwako kwa dakika 20 kisha nawa kwa maji ya vuguvugu.
Kwa maelezo zaidi na ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment