Saturday, 4 March 2017

Kitunguu swaumu kinafaida zake, lakini kikitumiwa vibaya huweza kuleta madhara haya

KITUNGUU swaumu ni miongoni mwa viungo vinavyotegemewa katika kuongenza ladha nzuri kwenye vyakula mbalimbali.

Mbali na kiungo hicho kutumika kunogesha vyakula pia kikitumiwa ipasavyo ni tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya.

Madhara ya kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu kama kikitumika bila maelekezo ya wataalam huweza kusababisha madhara yafuatayo:

Huweza kuchangia mhusika kuhisi kichefuchefu na wakati mwingine kutapika na kuharisha.

Pia huweza kusababisha hatari ya mhusika kuvuja damu kutokana na kuzuia seli sahani ambazo husaidia damu kuganda kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi wake wa kawaida.

Hivyo, kiungo hiki hakishauriwi kutumiwa kwa akinamama wajawazito au waliotoka kujifungua.

Kutokana na hayo ni vema ukaepuka kutumia kitunguu swaumu bila kupata ushauri kutoka kwa wataalam kwani huweza kuwa na madhara kwa afya yako.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nami kwa simu namba +255 716 300 200, +255 784 300 300, +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment