Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 17 March 2017

Kwa wale wenye maumivu wakati wa kukojoa wanaweza kutumia maua ya mlonge yatawasaidia

Mlonge ni mti ambao una asili ya India, lakini kwa sasa mti huu hupandwa kanda za Tropiki.

Karibu kila sehemu ya mti huu ni tiba yaani kuanzia mbegu zake, magome, majani, maua pamoja na mizizi. Sasa leo napenda uzifahamu baadhi ya faida za maua ya mti huo!!

Miongoni mwa faida za maua haya ni pamoja na kumsaidia mama anayenyonyesha kuongeza kiwango cha utokaji wa maziwa.

Sambamba na hayo, maua ya mlonge pia husaidia kutibu matatizo ya haja ndogo (mkojo) kutoka kwa shida au ukiambatana na maumivu, kwahiyo matumizi ya maua haya huweza kuondosha tatizo hilo.

Maandalizi ya maua haya ya mlonge katika tiba inabidi yachemshwe na kupata mfano wa chai iliyotokana na maua ya mlonge ambayo mhusika atahitajika kunywa chai hiyo kila siku kikombe kimoja asubuhi na jioni.

Hayo ndiyo machache ambayo nimeona nikwambie leo mdau wangu, lakini kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam  Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmanditz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment