Wednesday, 29 March 2017

Mambo 4 yatakayomfanya mwenzi wako atabasamu muda wote akiwa nawe


Kuna baadhi ya wanaume hudhani kuwa kujishusha kwa mawanamke na kumfanya atabasamu kwamba hiyo ni dalili ya udhaifu kwao au katika jamii kumbe si kweli kabisa.

Kwani hayo ni mambo ya kawaida kabisa katika mahusiano ya kimapenzi au kindoa kati ya mwanamke na mwanaume.

Sasa leo moja kwa moja tunaanza na wanaume ambapo tutaelekezana namna ya kumfanya mpenzi wako / mkeo atabasamu hata kama alikuwa amekasirika.

1. Omba radhi pale unapomkosea.
Unapofanya hivyo wewe mwanaume tambua kuwa utakuwa umejipandisha hadhi kwa mwanamke huyo na kuhisi kuwa unamthamini na kumjali pia mwanamke atajivunia kwa kuwa na mwanaume anayemheshimu na kutambua umuhimu wa fulaha kwake.

2. Onesha upendo wa dhati kwake muda wote
Hali hii unapaswa kuionesha kwa vitendo na kauli zako pia na unapaswa kuwa naye bega kwa bega kwa kila hatua anayoipitia katika maisha kwa kufanya hivyo lazima mwanamke ataishi na tabasamu muda wote katika ndoa au mahusiano hayo. 

3. Pale mwanamke anapokukera mweleze kwa hekima
Haimaanishi kila mwanamke anapokukosea anapaswa kufokewa au kumwagiwa lundo la matusi bali wewe kama mwanaume unapaswa kutumia maneno ya hekima katika kumueleza kuhusu kosa lake na ni vizuri umueleze mkiwa peke yenu na si mbele za watu au watoto kwani mwanamke atajihisi mnyonge na kukosa tabasamu pia.

4. Kuwa mtetezi wake
Unapoona mwanamke anakandamizwa au kuonewa wewe kama mwanaume unapaswa kuwa wa kwanza kuonesha upo upande wake na kumtetea. Mtete pale unapohisi thamani yake au utu wake unashushwa kwa makusudi, lakini jitahidi kufanya hivyo bila kusababisha ugomvi kati yako na aliyemkosea.

Kwa mengine mengi kama haya yanayohusu masuala ya mapenzi na mahusiano usiache kusikiliza kipindi cha NJOZI NJEMA  kila Jumatano saa nne usiku kupitia TBC FM hapo utakutana na Mtaalam Mandai pamoja na Salome Baptister na kuyajua mengi zaidi kuhusu mahusiano

Au wasiliana naye kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment