Tuesday, 28 March 2017

Mambo matano ya msingi unayopaswa kuyafahamu kuhusu faida za bilinganya

Bilinganya ni aina ya mboga ambayo inapatikana katika kundi la mbogamboga, lakini si mboga tu bali nayo inafaida zake kiafya.

Siku zote Mandai Products Company Limited tumekuwa tukiamini kwamba kila kitu kilichopo chini ya jua ni baraka ya mwenyezi Mungu na kinafaida yake kwetu sisi binadamu.

Kwa leo nimeona nikwambie hizi faida kadhaa za bilinganya kwako ni vyema ukazifuatilia hapa. Karibu>>

1. Kwanza matumizi ya bilinganya huwasaidia wale wenye shida ya kisukari kutokana na kwamba bilinganya zina 'carbohydrates' na soluble 'fiber' hivi vyote vinapopatikana ndani ya mwili basi husaidia sana kurekebisha kiwango cha sukari ndani ya mwili hususani kwa wenye kisukari type 2

2. Hulinda afya ya moyo, bilinganya inasifa ya kulinda afya ya moyo na kumsaidia mhusiaka kuepuka matatizo mbalimbali ya moyo. Bilinganya husaidia sana kuondosha cholesterol mwilini na kusimamia msukumo wa damu kuwa vizuri mwilini.

3. Pia matumizi ya bilinganya husaidia sana kuongeza madini chuma mwilini pamoja na kurekebisha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula na kuondosha matatizo ya kukosa choo.

4. Pamoja na hayo. inaelezwa kuwa matumizi ya bilinganya mara kwa mara huwasaidia wale watu wanaovuta sigara na wanahitaji kuacha kuvuta sambamba na kupambana na magonjwa sugu kama vile kiharusi.

5. Ndani ya bilinganya kuna 'antioxidants' ambayo husaidia pia  kupambana na maambukizi ya saratani.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment