Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 25 March 2017

Mambo matano yatakayokushangaza kuhusu faida za tangawizi

ginger root sliced
TANGAWIZI ni kati ya viungo mahili vinavyochochea ladha nzuri katika vyakula vya aina mbalimbali na hivyo kuwavutia walaji kula chakula husika.

Tangawizi pia inapowekwa kwenye vyakula vigumu kama nyama huifanya ilainike na hivyo kuweza kuiva kwa haraka zaidi. Hivyo kwa point hiyo tu kwanza utagundua kiungo hiki pia kinaweza kurahisisha umeng'enyaji wa chakula tumboni pia

Wakati tangawizi ikiwa inafahamika zaidi kama kiungo, kwa upande mwingine kiungo hicho huweza kupunguza athari za matatizo mbalimbali ya kiafya pia kama ifuatavyo kwenye orodha hii hapa chini:-

1. Hupunguza maumivu kwa wanawake wakati wa kipindi cha hedhi (Period)

2. Huppunguza maumivu ya mifupa pamoja na misuli kwa ujumla.

3.Inaelezwa kusaidia kuimarisha uwezo wa utunzaji wa kumbukumbu kwa binadamu.

4. Husaidia kutuliza maumivu ya tumbo pia

5. Husifika kwa kuimarisha kinga za mwili na kuufanya mwili kupambana vizuri dhidi ya magonjwa.

Kwa msaada zaidi au maelekezo kutoka kwetu kuhusu kutumia vizuri kiungo hiki tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment