Monday, 27 March 2017

Mambo mawili yanayoweza kutokea endapo mtu atakosa vitamin D


Kwa kawaida mwili huhitaji vitamin za aina mbalimbali ili kuendelea kubaki na afya bora na kinga kmara zaidi

Lakini leo naomba tuambiane mambo ambayo huweza kujitokeza kwenye miili yetu endapo itakosa vitamin D

Kwanza mtu mwenye upungufu wa vitamin D huwa katika hatari ya kuwa na mifupa isiyo imara hivyo anapopatwa na kashkash za hapa na pale huweza kuvunjika kirahisi kuliko mtu mwenye vitamin D ya kutosha.

Maumivu sugu ya viungo, Upungufu huu wa vitamin D huweza kupelekea tatizo la maumivu ya viungo ya mda mrefu endapo halitapatiwa ufumbuzi.

Pamoja na hayo, upungufu wa vitamini D pia huambatana na kukosa kupata jua la kutosha. na mara nyingi upungufu wa vitamini D umekuwa tatizo kubwa kwa wazee wasiojiweza, na kawaida kwa watoto na watu wazima.

Kuota jua ni moja ya njia rahisi ya watu kujitengenezea vitamini D hasa la asubuhi, Pia unaweza kuipata vitamin hiyo kwenye samaki, maziwa n.k

Kwa maelezo zaidi unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment