Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 7 March 2017

Mambo mawili yatakayoimarisha zaidi uhusiano wako na watu


Kuna baadhi ya watu katika maisha huwa ni muhimu kuwa nao na unapowakosa huweza kuwa na mapungufu fulani katika mambo yako ya kimaisha

Siku zote tambua kuwa uwezo wako binafsi au kipaji chako kunawakati kitahitaji kuwa na watu wa karibu ili kuweza kufika mbali zaidi.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia kutowapoteza watu wako muhimu katika maisha yako:-

1. Kuwa tayari kukosolewa
Acha kujifanya mjuaji wa kila kitu, kumbuka kuwa ushauri wa watu wengine pia unaweza kuwa na manufaa katika mambo yako/ kazi zako. Natambua kuwa kuna baadhi ya watu huwa hawahitaji kabisa kukosolewa wala kuwasikiliza wengine.

Kumbuka kuwa unapojifanya mjuaji wa kila kitu na hupendi kukosolewa itafika wakati kila watu watakuacha na hawatakwambia lolote hata pale watakapoona unaelekea kupotea.

2. Kuwa tayari kuomba msamaha
Tambua kuwa unapoomba msamaha haimaanishi kuwa wewe ni dhaifu bali ni hekima tu ambayo inaweza kukusaidia baadaye.

Kumbuka kuwa unapoomba msamaha unaongeza fursa ya kuimarisha uhusiano wako na watu wengine hasa wale ambao unawaomba msamaha.

Kwa maelezo zaidi au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment