Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 27 March 2017

Mambo ya msingi yakuyafahamu kuhusu nyanya leo

NYANYA ni moja ya tunda, lakini pia ni kiungo ambacho wengi wetu tumekuwa tukikitumia katika kuungia mboga ili kuongeza ladha ya chakula

Zipo faida kadhaa za kutumia nyanya kama tunda miongoni mwa faida hizo ni pamoja na:
Kuimarisha afya ya damu ndani ya mwili, hii ni kwasababu ndani ya nyanya kuna madini ya chuma ambayo husaidia kurekebisha afya ya damu mwilini.

Pia ndani ya nyanya kuna Vitamin K ambayo husaidia kudhibiti kutokwa kwa damu na kusaidia mzunguko wa damu ndani ya mwili.

Nyanya husaidia kulinda afya ya moyo, matumizi ya kiungo hiki huimarisha kiwango cha cholesterol kwenye damu . Hii ni kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘lycopene’.

Mbali na faidia hizo pia matumizi ya mara kwa mara ya nyanya husaidia kuboresha umeng’enyaji wa chakula ndani ya tumbo na hivyo kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa choo, lakini pia hata tatizo lakuhara.

Unaweza kuangalia hapa chini zaidi kuhusu umuhimu wa nyanya kiafya karibu:-

Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment