Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 15 March 2017

Matatizo matano ya kiafya yanayoweza kumalizwa na mdalasini kwa haraka


Mdalasini ni moja ya kiungo ambacho kinamama hukitumia sana kwa malengo yakuongeza ladha kwenye chai.

Lakini kiungo hiki hakiishii kuleta ladha nzuri tu kwenye chai bali pia ni mojawapo ya kinga na tiba ya magonjwa mbalimbali.

Leo ninayo orodha ya magonjwa ambayo huweza kuepukwa kwa kutumia kiungo hiki cha mdalasini. Karibu.
1. Kiungo hiki (mdalasini) kinauwezo wa kurekebisha kiwango cha sukari mwilini na hivyo kufanya kuwa na faida kwa wale wenye shida ya kisukari hususani kisukari aina ya pili 'type 2 diabetes'

2. Unapopata mafuta yatokanayo na huu mdalasini basi husaidia sana kuondosha shida ya fangasi hususani aina ya 'candida'

3. Pia matumizi ya mdalasini huweza kumkinga mtu dhidi ya saratani hasa saratani ya tumbo au saratani ya ngozi, uwezo huu ni kutokana na mdalasini kuwa na virutubisho hivi vya aina mbili yaani 'Cinnamaldehyde' na 'Eugenol' ambavyo vyote huweza kupambana vizuri na saratani.

4. Matatizo ya maumivu ya viungo nayo huweza kupata ufumbuzi kwa kutumia mdalasini hii ni kwa sababu kiungo hiki kinautajiri mkubwa wa madini ya magnesium ambayo pia uimarisha afya ya mifupa.

5. Mbali na hayo, kiungo hiki pia ni kizuri sana kwa kupunguza unene kutokana na kwamba kiungo hiki urahisisha mzunguko wa damu mwili na kuifanya damu kuzunguka vyema ndani ya mwili.

Kwa maelezo zaidi kuhusu  jinsi ya kutumia kiungo hiki kama tiba na kinga ni vyema ukawasiliana na Mtaalam Abdallaha Mandai sasa kwa simu namba: 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment