Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 23 March 2017

Matunda matatu usiyotakiwa kuyakosa kila siku


Ukweli ni kwamba kuna aina ya matunda mbalimbali ambayo yamekuwa na faida mbalimbali mwilini ikiwa ni pamoja na kujenga afya kwa ujumla.

Kwa ujumla matunda yamekuwa na sifa lukuki ndani ya miili yetu ikiwa ni pamoja na kuboresha afya ya ngozi zetu pamoja na kuimarisha kinga za mwili pia.

Hapa ninayo orodha ya matunda ambayo yanashauriwa kuliwa mara kwa na kuwa kutokana na kuwa na faida kadhaa mwilini

1. Parachichi


Hili ni tunda ambalo lipo tofauti sana na matunda mengine kutokana na kuwa na aina ya mafuta asili yenye kuleta afya mwilini pamoja na vitamin C na fiber.

Vitamini C iliyopo kwenye parachichi husaidia kuimarisha kinga za mwili na mafuta yatokanayo na tunda hili pia husaidia kuboresha afya ya ngozi pia.

2. Ndizi
Hili ni moja ya tunda lenye thamani pia kwani limesheheni madini ya 'potassium' pamoja na vitamin B6 na fiber pia.

3. Chungwa.
Tunda hili limekuwa likifahamika zaidi kwa kuwa na vitamin C nyingi na hivyo kuimarisha kinga za mwili zaidi.

Unaweza kujitahidi kupata tunda moja kila siku kati ya hayo hapo juu kila baada ya mlo wako ili kujenga afya yako zaidi.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment