Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 14 March 2017

Mwanamke mwenye dalili hizi 4 anaweza kupata shida kupata ujauzito

Picha kwa msaada wa mtandao
Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com ninayofuraha kukukaribisha kwenye muendelezo wetu wa kufahamishana taarifa mbalimbali hususani za afya.

Hapa leo ninazo dalili zinazoashiria mwanamke kushindwa kushika ujauzito. Karibu tuzifahamu.

Kwanza kabisa tatizo la kushindwa kushika ujauzito kwa mwanamke husumbua familia nyingi na husababishwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo upande wa wanaume.

Familia nyingi au wanandoa wengi huanza kuhisi tatizo hili baada ya kuishi katika mahusiano ya kutafuta ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mafanikio.

Ili mwanamke apate mimba ni lazima awe na sifa za kupata ujauzito, na ili mwanaume aweze kumpa mwanamke mimba ni lazima awe na sifa za kumpa mwanamke mimba, hivyo utaona kwamba matatizo haya huweza kuwepo kwa pande zote mbili au mojawapo.

Kutokana na kwamba tatizo hili huwahusu wanandoa wote wawili yaani mwanamke na mwanaume hivyo ni vyema wakati wa utafutaji wa ujauzito mwanamke na mwanaume wote kwa pamoja wakashirikiana kwani mwanaume unaweza kujiona huna tatizo kumbe ukija kupima mbegu zako utajikuta unatatizo kubwa.
Mwanamke mwenye tatizo la kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo haya yafuatayo;

1. Atakuwa amekaa na mume au yupo katika mahusiano ya kutafuta mtoto kwa zaidi ya mwaka lakini hakuna mafanikio, pia huweza kuwa analalamika maumivu ya chini ya tumbo mara kwa mara au yanaweza yasiwepo.

2. Lakini pia mwanamke mwenye tatizo la kutoshika ujauzito huweza kuwa na maumivu ya hedhi au kuvurugika kwa mzunguko na kutoona ute wa uzazi. hizo huweza kuwa moja ya viashiria vya tatizo hilo.

3. Pamoja na hayo pia wanawake wengi wenye shida hii ni nadra sana kuwa na hamu ya tendo la ndoa au kutojihisi raha wakati wa tendo na huhisi maumivu wakati wa tendo au kutokwa na uchafu ukeni wakati mwingine huambatana na muwasho na harufu.

4. Dalili nyingine za tatizo hili la kushindwa kushika ujauzito ni pamoja na kuwa na historia ya kuharibu au kutoka kwa mimba, historia ya kuzaa, au kufanyiwa upasuaji wa aidha uzazi au mirija. Ingawa wengine hawana historia hizi.

Ili kupata uhakika wa tatizo lako zaidi ni vyema kufika kwenye hospitali iliyokaribu nawe na kufanyiwa uchunguzi zaidi kabla ya kuanza matibabu ya aina yoyote.

Kwa ufafanuzi zaidi au msaada unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment