Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 4 March 2017

Picha maalum za kuhitimu elimu ya ujasiriamali


Washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Mandai Production Company Limited kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vyeti vyao na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo na Rais wa Shirika hilo la WUTA siku ya tarehe 04/03/2017 Jumamosi
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Mandai Production Company Limited kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) wakimsikiliza Mtaalam Mandai kwa umakini wakati mafunzo hayo yakiendelea


Mmoja wa wahiriki wa mafunzo hayo akijaribu kufumbua fumbo lililotolewa na Mtaalam Mandai kwa lengo la kupima uwezo wa kufikiri wa washiriki hao

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Mandai Production Company Limited kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) wakimenya nyanya tayari kwa kuanza mafunzo ya kutengeneza tomato sauce & tomato paste.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Mandai Production Company Limited kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) wakiosha nyanya za kutengenezea tomato sauce na tomato paste

Umenyaji wa nyanya za kutengenezea tomato sauce & tomato paste ukiendeleaUshirikiano wa washiriki wa mafunzo haya ulionekana kwa kiasi kikubwa hapa wakiwa wanaendelea kumenya nyanya kwa ajili ya kuandalia tomato sauce & tomato paste

Mkufunzi wa mafunzo hayo Mtaalam Abdallah Mohammed Mandai (Mwenye shati nyeusi) akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo wakati wakiendelea kuandaa viungo vya kuandalia tomato paste & tomato sauce.

Nyanya zikiendelea kumenywa 

Washiriki hawa wakipima kwenye mzan nyanya za kuandalia tomato sauce kabla ya kwenda kuzisaga

Zoezi la kusaga nyanya linaelekea kuanza sasa kwaajili ya kupata tomato sauce na baadaye tomato paste

Nyanya tayari zimeanza kusagwa na baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ili kupata tomato sauce na baadaye kufuatia  na tomato paste.

Kila mshiriki alipaswa kushiriki kila hatua ya kuandaa hii tomato sauce na tomato paste na hapa usagaji wa nyanya ukiendelea 

Nyanya tayari zimeshasagwa na sasa zipo jikoni kwa ajili ya kuanza kuchemka ili kupata tomato sauce 

Wakati zikiwa motoni kukorogwa muda wote ni muhimu ili kupata bidhaa bora zaidi hapa, Mtaalam Mandai mwenyewe akionesha namna sahihi ya ukorogaji wa nyanya hizo ili kupata tomato sauce nzuri zaidi.

Baada ya kuchemka kwa muda kuchuja pia ni muhimu ili kupata tomato sauce iliyo na ulaini wa kutosha na isiyo na mbegu  hapa washiriki hawa wawili walikuwa wakifanya zoezi hilo la uchujaji

Uchujaji wa tomato sauce ukiendelea 

Washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea kuandaa viungo vingine kwaajili ya kuchanganya kwenye tomato sauce ili kupata harufu nzuri na ladha nzuri kwenye tomto sauce,

Mtaalam Mandai akionesha namba ya kupima vitunguu swaumu kwaajili ya kuweka kwenye tomato sauce ili kuweka ladha ya bidhaa hiyo zaidi

Karafuu nayo ni moja ya kiungo ambacho huhitajika kwenye uandaaji wa tomato sauce hapa Mtaalam Mandai akipima kwa kutumia kijiko kidogo

Viungo kama kitunguu maji, kitunguu swaumu na karafuu, pilipili vikisangwa kwa pamoja kwaajili ya kuchanganya kwenye nyanya ambazo tayari zimeshaanza kuchemsha ili kupata tomato sauce.

Mmoja wa washiriki akiweka tomato sauce ndani ya chupa baada ya kukamilika maandalizi yake na kuiva na sasa itakuwa  tayari kwa ajili ya matumizi au kuingizwa sokoni

Mtaalam Mandai (Mwenye shati nyeusi) akionesha namna ya kuweka 'label' kwenye chupa yenye tomato sauce mara baada ya kukamilika

Baada ya mafunzo washiriki walipata muda kidogo wa kupata chakula kwenye mgahawa wa Mandai Natural Food uliopo Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege ambao pia unamilikiwa na Mtaalam Mandai

Mmoja wa washiriki wakipata chakula ndani ya Mandai Natural Food 


Mshiriki wa mafunzo hayo akiwa anapata chakula ndani ya Mandai Natural Food
 Zifuatazo ni picha zinazoonesha washiriki wote wakipatiwa vyeti vyao na Mkurugenzi wa Mandai Products Company Limited na Rais wa WUTA


Mmoja wa washiriki akisaini kitabu baada ya kupokea cheti chake kwa mhasibu Richard Mbena

Utiaji wa saini mbele ya mhasibu Richard Mbena ukiendelea baada ya washiriki kukabidhiwa vyeti vyao
Baadhi ya washiriki wakipata maelezo mafupi kutoka kwa mtaalam wa kuandaa label Ndugu Hashim Zungu kutoka Mandai Production Company Limited

Hashim Zungu Mtaalam wa kuandaa label kutoka Mandai Production Company Limited akiwaonesha baadhi ya washiriki moja ya label za tomato sauce inavyoonekana baada ya kuwekwa kwenye bidhaa.
Kwa ushauri zaidi au maswali kuhusu biashara au ujasiriamali unaweza kutupigia simu kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au fika ofisini kwetu Ukonga, Mombasa eneo la Mongolandege tutakusaidia 

No comments:

Post a Comment