Tuesday, 21 March 2017

Sababu 4 kwanini wanawake wengi huongezeka uzito mara baada ya ndoa


Asilimia kubwa ya wanawake wanaoingia kwenye ndoa ghafla huongezeka uzito na baadhi ya kupoteza kabisa muonekano wao kabisa.

Sasa leo napenda kukueleza baadhi ya sababu ambazo huchangia wanawake wengi kunenepa au kuongezeka uzito mara baada ya kuingia rasmi kwenye ndoa zao.

1. Mtindo wa ulaji hubadilika.
Wengi hubadili mtindo wa ulaji na hasa ule mwanzo wa ndoa unakuta karibu kila kitu huwa rahisi kupatikana hivyo huwa rahisi hata kupata aina zote za makundi ya vyakula na hivyo kuchangia hata uzito kuongezeka kwa wanawake wengi.

2. Ulaji wa mara kwa mara.
Mara nyingi wanawake wanapoingia kwenye ndoa huwa na mda mrefu wa kupumzika nyumbani na hivyo kujikuta karibu siku nzima wanashinda wakiwa wanakula, hali ambayo huchangia kuongezeka kwa uzito wao pia

3. Huwa na muda wa kupumzika
Kipindi cha awali cha ndoa kinamama wenge hupata muda wa kutosha wa kupumzika ambao unaweza kufika hata mwezi mmoja tofauti na wanaume ambao wao mara baada ya ndoa tu huhitajika kurejea katika majukumu ya kila siku hasa yale ya kikazi. Hivyo hii nayo ni moja ya sababu inayochangia wanawake wengi kuongezeka uzito mara baada ya ndoa.

4.Kukosa msongo wa mawazo
Mwanzoni mwa ndoa nyingi huwa hakuna changamoto zozote mara nyingi, hivyo hali hiyo hutoa nafasi kwa wanawake wengi kuridhika na kujikuta wakiongeza uzito wa miili yao.

Kama unasumbuliwa na tatizo la uzito mkubwa unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment