Tuesday, 7 March 2017

Sababu kuu 2 zinazokufanya usifikie mafanikio yako kimaisha


Naamini wewe kama binadamu lazima kuna wakati utakuwa umewahi kujikuta ukijiwekea malengo yako halafu ukashindwa kabisa kuyatekeleza kutokana na sababu mbalimbali ambazo unadhani kwako zilikuwa na msingi.

Leo nataka kukueleza haya mambo mawili ambayo huchangia malengo ya watu wengi kutokamilika katika maisha yao na kubaki kulalamika karibu kila siku.

1. Kutokujiamini
Kuna watu wengiambao wanatamani kufanya mambo makubwa sana lakini hushindwa kuyatimizi kutokana na kutokujiamini kabisa kuwa wanaweza kufanya.

Baadhi ya watu wanamawazo mazuri na makubwa endapo yatafanyiwa kazi lakini hujikuta wakishindwa kuyatimiza kutokana na kusongwa na hali ya kutokujiamini yaani wanaogopa kushindwa na kuhisi uenda watu watawacheka au kuwazungumzia vibaya hali ambayo imechangia kufukia ndoto za watu wengi hadi sasa.

Siku moja kaa ufikiri kwa umakini kuhusu mipango yako mingi uliyonayo kichwani mwako, lakini bado hujawahi kuifanyia kazi kwa sababu ya kuogopa kushindwa. Pia fikiria endapo ungeamua kuifanyia kazi mipango yako yote ungekuwa wapi hadi sasa naamini ungekuwa mbali zaidi.

Unachotakiwa kuelewa kuanzia sasa ni kwamba mafanikio katika jambo lolote lile hutegema ujasiri wako na si uoga wako. Kumbuka kuwa mambo mengi ambayo unayaogopa kuyachukulia hatua sio magumu kama unavyohisi. Chukua hatua leo.

2. Kughairisha mambo
Watu wengi sana wamekuwa na kijitabia hiki na kuendekeza neno kesho, wao kila kitu utasikia nitafanya kesho au wiki ijayo, mwezi ujao na hata mwaka ujao bila kujali kuwa wanachelewesha mafanikio yao wao wenyewe.

Acha kuendekeza neno kesho hebu anza leo kutimiza mipango yako uliyojiwekea ya kujikwamua kiuchumi na utaona mabadiliko kama utaamua kwa dhati kabisa kutoka moyoni.

Unaweza kunipigia simu kwa ushauri zaidi wa kimaisha pamoja na masuala ya lishe bora na asili kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment