Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 15 March 2017

Ufuta husaidia kuondoa maumivu ya hedhi kwa wanawake


Kwa kawaida kila mwanamke hupitia hali ya kupatwa na hedhi kila mwezi, ikiwa ni hali yao ya kawaida kutokana na Mungu alivyowaumba.

Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wanapokuwa ndani ya siku hizo.

Hapa ninazo njia 3 ambazo huweza kusaidia kumaliza tatizo hilo.

1. Ufuta
Ufuta ni mbegu za asili ambazo huweza kutumika kwa kupunguza maumivu wakati wa hedhi, unachopaswa kufanya ni kusaga ufuta kisha tumia unga wake na utakusaidia.

2. Tangawizi
Kiungo hiki nacho husaidia kupunguza maumiwa ya wakati wa hedhi, unaweza kutumia siku mbili kabla ya kuingia katika mzunguko wako ili kupata matokeo mazuri zaidi.

3. Papai
Papai hususani lile bichi pia huweza kuwa moja ya suluhisho ya tatizo ya maumivu wakati wa hedhi kwani husaidia kulainisha misuli ya sehemu za uzazi na hivyo kusaidia kupunguza maumivu wakati wa hedhi.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment