Tuesday, 21 March 2017

Ukiona mambo haya 7 kazini kwako basi usikubali kuendelea na kazi hiyo


Kazi ni muhimu kwa kila binadamu katika kutimiza yale mahitaji muhimu ya kimaisha na familia kwa ujumla.

Lakini kuna baadhi ya mambo unapoona yanatawala zaidi kichwani mwako au katika mawazo yako basi tambua kuwa kazi unayofanya haikufai na unastahili kuacha na kutafuta kazi nyingine ambayo inaweza kukufaa zaidi.

Zifuatazo ni dalili zinazoonesha kuwa kazi unayoifanya unastahili kuachana nayo:-

1. Ukiona unapata shida kwenye kuamka asubuhi.
Hii ni dalili ya kwanza kabisa kwamba kazi unayoifanya hustahili kuendelea nayo, kwani kwa kawaida kazi unayoipenda lazima utakuwa na moyo hata wakati wa kuamka asubuhi bila kuona uvivu wowote.Hivyo ukiona hali hiyo tambua kuwa kazi hiyo unayoifanya unastahili kuacha na hata kama utaendelea nayo hautakuwa na ubunifu nayo.

2. Kazi unayofanya inaathiri afya yako.
Tambua kuwa hainamaana kuendelea kufanya kazi eneo ambalo unaharibu afya yako kwahiyo unapogundua umekuwa ukipatwa na matatizo kadhaa ya kiafya kutokana na kazi yako ni vyema kuondoka mara moja na kutafuta sehemu nyingine ya kazi ambayo itakuwa rafiki kwa afya yako

3. Unafanya tu kwaajili ya kupata fedha
Ukiona upo sehemu unafanya kazi tu kwaajili ya kupata mshahara mwisho wa mwezi basi tambua kazi hiyo haikufai kwani huwezi kuonesha ubunifu wowote katika majukumu yako kwa sababu wewe upo hapo kwaajili ya kupata fedha tu kila mwisho wa mwezi pasipo kutimiza majukumu yako.

4. Huna jipya kila siku
Ukiona kila siku unafanya kazi zako kwa mtindo ule ule na utaratibu ule ule basi jua hicho unachokifanya hakikufai na unatakiwa kuachana nacho. Kwani kwa kawaida mtu anayependa kazi yake karibu kila siku huja na mawazo mapya ya kuboresha kile anachokifanya.

5. Hauendi sawa na bosi wako
Kama upo kazini na hauna maelewano mazuri na bosi wako basi tambua kuwa haina haja ya kuendelea kufanya kazi eneo hilo, kwani usitegemee kufanikiwa katika eneo hilo labda endapo utajitahidi kurekebisha kwanza uhusiano wako na bosi wako ndio utaweza kufanikiwa nawe pia.

6. Ukiona haufiti kwenye nafasi yako
Unapoona unafanya kazi miaka miwili au mitatu, lakini bado umeshindwa kutimizi majukumu yako kama unavyotakiwa kufanya basi tambua kasi hiyo hautakiwi kuendelea nayo kwani hautaweza kuifanya vile inavyopaswa hata mara moja na ni bora ukaacha na kutafuta sehemu ambayo utafiti vizuri.

7. Unatumia muda mwingi kufika kazini kwako
Kama unapoishi na kazini kwako kuna umbali ambao kila siku lazima utumia zaidi ya saa 5 kwenda na kurudi basi hiyo sehemu ya kazi itakuwa haikufahi na utahitaji kutafuta kwingine ambapo ni karibu kidogo na unapishi. Kwa sababu kama unatumia mda mrefu pia unatumia pesa nyingi hivyo hivyo kila siku katika kwenda na kurudi hivyo kwa mtindo huo hautakuja nufaika na kazi yako zaidi ya kupata ela ya kula tu.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment