Saturday, 11 March 2017

Ukiona unahofu ya kutimiza kila lengo lako,jaribu kutumia mbinu hizi 3


Inawezekana tangu mwaka huu uanze umekuwa na malengo yako kadhaa ambayo ulijiwekea, lakini huenda umejikuta hadi sasa hakuna dalili yoyote ya kutimiza hata lengo moja na miezi ndio hiyo inazidi kuyoyoma.

Hivyo basi kama wewe ni mmoja wa watu wenye shida hii ya kupanga malengo mara kwa mara na huwa hayakamiliki naomba nikupatie mbinu hizi kadhaa ujaribu kuzitumia na naamini zinaweza kukufaa zaidi.

1. Badilisha mikakati yako.
Kwa kawaida unapopanga kufanya jambo fulani lazima uwe na mikakati ya namna ya kulitekeleza sasa inawezekana aina ya mikakati unayoitumia ndio tatizo au kikwazo katika malengo yako.

Kuanzia sasa jitahidi wakati wa kuweka mikakati ya malengo yako hakikisha inaendana na mazingira ya lengo unalohitaji kulitimiza, lakini pia hakikisha mikakati yako inakikomo cha muda wa kutimiza lengo husika.

2. Ondoa hofu 
Baadhi ya watu huwa na malengo mazuri, lakini hujikuta wakisumbuliwa na hofu kwani wengine hujikuta wakiogopa labda watu wake wakaribu watamuonaje endapo wakigundua kuwa yeye kwa sasa ameamua labda kuuza nyanya au ameamua kuwa mkulima wa kilimo cha umwagiliaji.

Siku zote shikiria kila unachokiamini katika maelengo yako na usiangalie watu wa pembeni yako watazungumza nini kuhusu ilo lengo lako.

3.Kuondokana na hali kukata tamaa.
Watu wengi wameshindwa kufikia malengo yao katika maisha kwa sababu ya kukata tamaa mapema. Hapa inawezekana wao wenyewe kujikatisha tamaa au wakati mwingine watu wa karibu huweza kuwashinikiza kukata tamaa.

Hata kama unapitia changamoto nyingi kiasi gani yakupasa kuzivumilia na kuendelea kuamini katika lengo lako hadi uone mwisho wake.

Kwa ushauri zaidi usisite kutupigia simu kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Kumbuka tupo kwa ajili yako msomaji wetu.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment