Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 18 March 2017

Usikubali zikupite hizi faida 4 za juisi ya boga leo


Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com imani yangu kwamba unaendelea vizuri popote pale ulipo unaposoma makala hii.

Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti yetu hii basi utakumbuka kuwa tayari tumewahi kuzungumza mara kadhaa kuhusu faida za mbegu za boga, lakini leo napenda tuzungumze kuhusu faida za juisi yake.

Najua kwa baadhi ya watu itakuwa ni jambo la kushangaza kusikia kuhusu juisi ya boga lakini hakuna kitu ambacho kinashindikana chini ya jua.

Zipo faida kadhaa za matumizi ya juisi ya boga na hapa napenda kukufikishia hizi baadhi>>>>>>
Juisi ya boga inauwezo mzuri wa kupambana na shinikizo la juu damu pale unapokunywa mara kwa mara hii ni kwa sababu ndani ya boga kuna kirutubisho kiitwacho 'pectin' ambayo hufanya kazi ya kushusha cholesterol na hivyo kupambana na matatizo ya shinikizo la damu.

Huimarisha kinga za mwili, juisi ya boga ina virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini pamoja na vitamin, ambavyo ni muhimu sana kwa kuimarisha kinga za mwili ndani yetu.

Juisi ya maboga haisaidii tu shinikizo la damu na kuimarisha kinga za mwili bali husaidia sana kumkinga mhusika dhidi ya matatizo ya shambulio ya moyo pamoja na kiharusi 'stroke'

Aidha, matumizi ya juisi hii ni muhimu sana kwa afya ya figo na ini katika hili juisi hii itakusaidia zaidi pale unapokunywa mara tatu kwa siku yaani asubuhi mchana na jioni kila siku kwa kufanya hivyo husaidia hata kuondosha mawe kwenye figo.

Pamoja na hayo, juisi hii ni nzuri kwa kurekebisha mmeng'enyo wa chakula tumboni,'digestion system' kutokana na kuwa na kiwango cha nyuzinyuzi 'fiber' za kutosha hivyo juisi hii ni kinga tosha ya matatizo kukosa choo mara kwa mara.

Mbali na hayo, juisi hii pia inauwezo wa kuwasaidia wale wenye uhitaji wa kupunguza miili pamoja na kuboresha afya ya ngozi pia.

Ndugu msomaji wangu hizo ni faida kadhaa za matumizi ya juisi ya boga, napenda kukuahidi kwamba bado ninazo faida nyingine za juisi hii kama ungependa kuzijua nipigie kwa simu namba 0716 300  200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment