Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 7 March 2017

Viungo vitatu vyenye uwezo wa kupunguza maumivu ya mwili

Miongoni mwa matatizo ambayo huwakumbuka watu wengi ni pamoja na hili tatizo la maumivu ya viungo mwilini.

Naamini unaweza kuwa wewe ni miongoni kati ya watu ambao kuna baadhi ya siku umeamka na kujikuta unamaumivu sehemu mbalimbali za mwili wako.

Maumivu hayo ya viungo huweza kusababishwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchovu wa kazi, safari na wakati mwingine huwa ni moja ya dalili za magonjwa fulani fulani.

Leo napenda tufahamu hivi viungo vya aina tatuvi ambavyo huweza kusaidia kupunguza tatizo hilo.

Tangawizi
Kiungo hiki ni muhimu pia kwa kupunguza maumivu ya viungo mwilini kutokana na kiungo hicho kuwa na uwezo wa kurahisisha mzunguko wa damu kwenda vizuri ndani ya mwili. Hivyo matumizi ya kikombe kimoja cha tangawizi kila siku huweza kuwa msaada kwako ikiwa unatatizo la maumivu ya viungo.

Mdalasini
Kama una maumivu ya viungo pia unaweza kutumia kiungo hiki ambapo unaweza kunywa maziwa yalichanganywa kidogo na mdalasini pamoja na asali kidogo na utaona faida yake.

Binzari
Kiungo hiki kinafahamika sana kwa akina mama na wengine hukifahamu kwa jina la manjano, ili kiungo hiki kiwe msaada kwa tatizo hili utahitajika kupata maziwa kisha changanya na kijiko kidogo cha binzari baada ya hapo chemsha kwa pamoja kisha subiri yapoe kiasi, lakini yasipoe kabisa halafu utatumia pamba kuchua sehemu yenye tatizo.

Hayo ni machache tu, kwa mengi zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 784 300 300, +255 769 400 800.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment