Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 22 March 2017

Wanawake: Njia 7 za asili zitakazofanya uwe na miguu mizuri


Wengi wetu tumekuwa tukithamini baadhi ya sehemu za viungo vyetu mwilini, lakini miguu tumekuwa tukiisahau kuitunza vizuri.

Angalau kidogo kwa wanawake wao hujitahidi zaidi kuhusu utunzaji wa miguu yao, lakini kwa wanaume ni nadra sana kuzingatia usafi na afya ya miguu yao na ndio maana asilimia kubwa ya matatizo ya fangasi za miguu huwakumba zaidi wanaume kuliko kinamama.

Hapa ninazo mbinu kadhaa ambazo zinaweza kusaidia utunzaji wa miguu yako ukiwa nyumbani pasipo gharama yoyote.

1.Hakikisha muda wote miguu yako ni misafi na yenye ukavu wa kutosha ili kuepuka kupatwa na matatizo ya fangasi na miguu kutoa harufu pia

2. Osha miguu yako vizuri, tafuta kitu kizuri cha kusugua miguu yako ambacho hakitaathiri ngozi ya miguu yako na utumie kila unapooga kwa kusugua miguu yako.

3. Lainisha miguu yako kila siku kwa mafuta mazuri ikiwezekana yawe ya maji yanaweza kuwa ya nazi kwa matokeo mazuri zaidi.

4.Hakikisha unasugua vizuri miguu yako sehemu za kisigino kwa jiwe maalum ili kuepusha miguu yako kupasuka.

5. Jiwekee utaratibu wa kuloweka miguu yako kwenye maji ya uvuguvugu angalau kwa dakika 10 hadi 15. Fanya zoezi hilo kwa mwezi mara moja ili kuboresha afya ya miguu yako.

6.Vaa soksi hata kama upo nyumbani tu hii husaidia kuzuia miguu kupatwa na vumbi na wadudu wengine wadogowadogo.

7. Epuka kuvaa viatu vya kubana sana hii huweza kuchangia majeraha madogomadogo hasa kwenye kidole gumba . Halikadhalika unashauriwa pia kuepuka kuvaa viatu virefu kwani huchangia maumivu ya miguu pia .

Kwa mawasiliano zaidi tupigie kwa simu nanmba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 784 300 300.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment