Friday, 14 April 2017

Acha kutupa ganda la ndizi kuanzia leo, zipo faida zake 3 hapa


Kuna baadhi ya mambo ukiambiwa leo unaweza ukahisi unadanganywa na usitake kuamini hata kidogo, lakini ni ukweli yapo.

Mfano leo msomaji wangu nikikueleza kuwa yale maganda ya ndizi mbivu ambazo huwa tunatupa yanweza kutumika kwa kazi nyingine je, unaweza kuniamini?Najua wengi watasema hapana, lakini ni ukweli yale maganda yanaweza kuwa na matumizi mengine zaidi ya kuyatupa.

Zifuatazo ni faida za ganda la ndizi:-

1.Husaidia kung'arisha meno
Chukua sehemu ya ndani ya ganda la ndizi na kisha sugulia kwenye meno itasaidia kuyafanya meno yako kuwa meupe

2.Husaidia kuondoa vipele vya mbu na wadudu
Tumia ganda la ndizi kwa kusugulia sehemu uliyoumwa na mdudu au mbu ili kuondoa  maumivu na wekundu.

3. Huondoa mikunjo usoni ( wrinkles)
Changanya ute wa yai na nyuzi nyuzi za ndani ya ganda la ndizi kisha paka usoni kwa dakika 20, ili kupoteza mikunjo.
Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment