Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 12 April 2017

Aina 3 za vinywaji muhimu kwa mama mjamzito

Picha kwa msaada wa mtandao
Mama mjamzito anapaswa kutazwamwa kwa upekee sana wakati wote wa kipindi cha ujauzito ili kuweza kufahamu maendeleo na ukuaji wa mimba.

Moja ya mambo muhimu ya kuzingatia kwa mama mjamzito akiwa katika hali hiyo ni pamoja na ulaji na vinywaji mbalimbali.

Leo naomba nikuelezea hizi aina kadhaa za juisi ambazo hupendekezwa kwa mama mjamzito:-

Juisi ya karoti
Juisi hii humsaidia mama mjamzito kwenye upande wa mmeng'enyo wa chakula na hivyo kumuepusha mama dhidi ya ukosefu wa choo kama ilivyo kwa wajawazito wengi.

Pia juisi hii husaiida kuboresha ngozi ya mama mjamzito kwani baadhi ya kinamama wakati wa ujauzito huharibika ngozi zao.

Juisi ya tango
Juisi hii pia ni muhimu kwa mama mjamzito kwani husaidia kulinda afya ya fizi na meno

Juisi ya boga
Juisi hii husaidia kumuepusha mama dhidi ya kisukari cha mimba pamoja na ukosefu wa choo na kupunguza uwezekano wa shinikizo la juu la damu.

Juisi nyingine muhimu kwa mama mjamzito ni pamoja na juisi ya chungwa, apple n.k

Kwa ushauri na ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment